Licha ya kukabiliwa na shinikizo la kupanga tarehe ya uchaguzi, Rais wa Senegal, Macky Sall amesema ataachia madaraka ifikapo April 2, 2024 wakati ambao muda wake wa uongozi unakoma huku akisema anafikria kuwaachia huru viongozi wa Upinzani walio kizuizini.
Shinikizo hilo la kupanga tarehe ya kupiga kura, limemkumba Sall baada ya kuucheleweshwa kwa uchaguzi uliotarajiwa kufanyika Februari 25, 2024 hali iliyosababisha maandamano kwa wiki kadhaa.
Amesema, hatotangaza tarehe mpya ya uchaguzi mpaka baada ya mazungumzo ya kisiasa yanayotarajiwa kuanza wiki ijayo kujadiliana na wagombeaji urais na wahusika wengine wa kisiasa na kijamii nchini humo.
Aidha, Rais Sall pia amesema anafikiria kuwaachilia huru viongozi wa upinzani, Ousmane Sonko na Bassirou Diomaye Faye walio kizuizini.)