Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekemea uzembe unaofanywa na baadhi ya watumishi wanaochelewesha huduma kwa Wananchi, ikiwemo kubadili transfoma zinazopigwa radi hasa katika mkoa wa Njombe.

Kauli hiyo ya Dkt. Biteko ameitoa katika ziara yake katika mkoa wa Njombe jimbo la Wanging’ombe kufuatia changamoto iliyowasilishwa na mbunge wa jimbo la Wanging’ombe ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange ambaye amesema mkoa wa Njombe unachangamoto ya radi ambazo zinapiga transfoma na kusababisha mgao hivyo kukwamisha shughuli za uchumi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe hususan ni Wanging’ombe.

Amesema, “tunachangamoto kubwa ya radi kwa mwaka tunaweza kubadilisha transfoma 50,60 na kuendelea na mara nyingi transfoma ikiharibika inachukua miezi kadhaa umeme kuja kwa wananchi hii inaleta kero tunaomba transfoma zinanoweza kuhimili geografia Wanging’ombe na mkoa mzima wa Njombe.”

Akijibu hoja hiyo, Dkt. Biteko amesema “Mbunge amesema transfoma ikiungua inachukua mwezi mmoja kubadilishwa uzembe huo hatuukubali na pale Tanesco makao makuu kuna watu walishazoea matatizo haiwezekani transfoma inaungua hakafu inachukua mwezi mzima ndio maana idara ya manunuzi pale Tanesco niliwambia wawabadilishe.”

Rais Sall afikiria kuwaachia Viongozi wa upinzani
SMZ kupunguza makali bei za Vyakula