Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itapunguza gharama za vyakula nchini.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Msikiti wa Mubarak Bububu Kihinani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema atatoa taarifa muda mfupi ujao katika kukabiliana na hali ya upandaji wa gharama za vyakula, ili kuwapunguzia mzigo wananchi.

Aidha Dkt. Mwinyi pia amewahimiza waumini kutenda mema kwa kudumisha amani na kuwasaidia makundi ya wasiojiweza katika kuelekea kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Seikali yakemea ucheleweshaji huduma kwa Wananchi
El-Shadai yawashika mkono waathiriwa Hanang'