Scolastica Msewa, Mkuranga – Pwani.

Miradi 13 imezinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani, yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 10.2.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Hadija Nassir Ally ameyasema hayo wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru huko Kipala mpakani katika Kata ya Mwandege Wilayani Mkuranga ukitokea wilaya ya Kisarawe.

Alisema Mwenge huo wa Uhuru utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 ya sekta ya afya, elimu, maji na bustani ya Miche ya misitu, shughuli za ujasiriamali wa vijana, uzinduzi wa darasa la utoaji wa elimu ya mapambano kupingwa na kuzuia vitendo vya rushwa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024, Godfrey Mzava amepongeza uongozi wa Wilaya ya Mkuranga kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo sambamba na umakini wa usimamizi wa fedha zinazoletwa wilayani humo.

Aidha alitoa pole kwa Wananchi walioathirika na mafuriko katika Wilaya hiyo ya Mkuranga na kuwataka kuendelea kuchukua tafadhali kwa kusikiliza maagizo ya serikali kwa kuhama katika maeneo hatarishi.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega alisema kupitia Mwenge huo miradi ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 imekaguliwa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 6, 2024
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 5, 2024