Wengi wa Wagombea wa uchaguzi ulioahirishwa nchini Senegal na Jumuiya za kiraia, kwa pamoja wamesema hawatashiriki mazungumzo yaliyopendekezwa na Rais Macky Sall ya kuamua tarehe ya upigaji kura ambao aliuahirisha mapema mwezi huu.
Wakiongea na Vyombo vya Habari. Viongozi hao akiwemo Boubakar Camara wamesema, wanapinga mapendekezo ya mdahalo na wanataka tarehe ipangwe kabla ya Aprili 2, 2024.
Sall amekuwa akipambana na ongezeko la wito wa kumtaka atangaze siku ya uchaguzi wa rais, baada ya kuuahirisha ghafla uchaguzi wa Februari 25 na kusababisha mgogoro wa kisiasa kwa wiki kadhaa.
Katika mahojiano na Vyombo vya Habari, Sall hakuzungumzia uamuzi wa kutaja tarehe, akidai mpaka baada ya mazungumzo na wanasiasa na watendaji wa kijamii yatakapofanyika.