Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mary Maganga ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa – BMH kwa utoaji huduma bora za afya.

Ametoa pongezi hizo jijini Dodoma wakati alipokutana na uongozi wa Hospitali hiyo ya umma inayohudumia Kanda ya Kati na Mikoa ya jirani.

Amesema, “tumekuwa tukipata huduma hapo kwenu (BMH) na tunapata huduma nzuri tu pasipo kujieleza kuwa tunatoka ofisi gani.”

BMH ilipata pongi hizo mara baada ya  kumtembelea Katibu Mkuu ofisini kwake iliopo mji wa Serikali Mtumba, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt Alphonce Chandika.

“Nawapongeza kwa kutunza mazingira ya Hospitali vizuri. Ni taasisi ya umma ambayo imepanda miti mingi pia majiko ya kantini zenu hamtumii majiko ya mkaa,” amesema Katibu.

Wapinzani wasusia wito wa Rais kupanga tarehe ya uchaguzi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 24, 2024