Scolastica Msewa, Chalinze – Pwani.

Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amepokea na kuzindua Mradi wa Umeme wa Sola katika Shule ya Sekondari ya Jakaya Mrisho Kikwete wenye thamani ya zaidi ya milioni 16 huko Msolwa Chalinze mkoani Pwani uliotolewa na Kampuni ya Matheostechs kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Ridhiwani amepokea na kuzindua Mradi huo katika Shule mpya ya Jakaya Mrisho Kikwete ambayo imejengwa kwa lengo la kusogeza Shule kwenye kijiji ambacho wanafunzi wake walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata elimu.

Amesema, shule inayoendelea kujengwa ina miundombinu mizuri lakini hakukuwa na umeme lakini kwa ushirikiano wa Kampuni ya Matheostechs wakesaidia kumaliza tatizo la kukosa Umeme shuleni hapo.

Aidha amewataka Wanafunzi, Walimu na Wazazi kuisaidia kutunza miundombinu mizuri ya mfumo wa umeme huo, sambamba na kuwataka Wanafunzi kusoma kwa bidii kwa lengo la kuenzi jina kubwa la Jakaya Mrisho Kikwete.

Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Matheostechs Theobald Bonaventure alisema Kampuni yake iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni kushiriki jitihada za kuboresha sekta ya elimu nchini na kuenzi jina la Jakaya Mrisho Kikwete.

Waliofariki ajali ya Lori Arusha wafikia 25
Meno ya Tembo yamtokea puani Mahmoud