Johansen Buberwa – Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, linamshikiria mtu mmoja, Edson Mahmoud (44), mkulima Mkazi wa Kitongoji cha Kafua kilichopo Kata ya Nyamihaga Wilayani Ngara Mkoani Kagera, kwa kukutwa na vipande vitatu vya Meno ya Tembo.

Akizungumza na vyombo vya Habari Ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera Blasius Chatanda amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa na meno hayo Februari 21, 2024 majira ya saa nne asubuhi, katika Kata ya Benako Wilayani humo, akiwa na vipande vya Meno hayo vinavyo kadiriwa kuwa na uzito wa kilogram 12, akisafirisha kwenda kuviuza kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajiri MC 977 DGZ aina ya Bajaji Boxer.

Amesema, jeshi hilo linaendelea na msako mkali ili kuwakamata wengine waliotoroka na kuwafisha kwenye vyombo vya sheria na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Aidha, Polisi pia imetoa onyo kwa watu wote wanaoendelea kujihusisha na njia haramu za kujipatia kipato na kuwataka kuacha mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mradi Umeme wa Sola waifikia Sekondari ya Jakaya Kikwete
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 25, 2024