Abel Paul, Jeshi la Polisi – Arusha.

Takribani watu 25 wamefariki dunia, huku wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Ngaramtoni kibaoni by Pass, ikihusisha Lori na magari mengine madogo matatu Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha.

Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji akiwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru amesema ajali hiyo ilitokea Februari 24, 2024 muda wa saa 11:00 jioni katika Barabara ya Arusha Namanga, kwa kuhusisha lori hilo lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba za usajili ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi Nchini Kenya.

Amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni Wanaume 14, Wanawake 10 na Mtoto mmoja wa kike na kufanya jumla yao kufikia 25, huku idadi ya raia wa kigeni waliofariki ikiwa ni watu saba.

Katika ajali hiyo, majeruhi hao 21 kati yao Wanaume ni 14 na Wanawake ni saba, huku magari yaliyopata ajali katika tukio hiloyakiwa ni yale yenye namba za usajili T 623 CQF aina ya Nissan Caravan, T 879 DBY aina ya Mercedes Benz Saloon na T 673 DEW aina ya Toyota coaster mali ya shule ya (New Vision School).

Aidha, Kamishna huyo wa opereshini na mafunzo ya Jeshi la Polisi nchini amekitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa kuwa ni kufeli breki ya lori, kitendo kilichopelekea kuyagonga magari mengine na kwamba bado wanaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha ajali hiyo, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

 

Ustawi wa maisha umechangiwa na waliotangulia
Mradi Umeme wa Sola waifikia Sekondari ya Jakaya Kikwete