Kocha Mkuu wa CR Belouizdad, Marcos Paqueta ameondoka, huku akiwalalamikia kiungo wa Young Africans Pacome Zouzoua na Stephanie Aziz KI, kwa kusema ndio waliowaharibia timu yao na kupata kipigo kikubwa.
CR Belouizdad, ilikumbana na kisago kizito juzi Jumamosi (Februari 24) katika uwanja Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kwa kufungwa mabao 4-0, katika mchezo wa Mzunguuko watano wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Akizingumza kabla ya kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea Algiers – Algeria, Paqueta amesema hatua ya viungo wake na mabeki kushindwa kumdhibiti ZouZoua lilikuwa kosa kubwa lililowapa wakati mgumu kwenye mchezo huo.
Paqueta amesema Pacome alikuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo na mapema walishajipanga kumdhibiti lakini hesabu zao hazikufanikiwa kutimia baada ya awali kushtukia makali yake.
“Yule weye jezi namba 26 (1Pacome) ndiye aliyefanya kazi kubwa kwenye mchczo huu, alituweka kwenve wakati mgumu sana licha ya kwamba tulishajipanga kuhakikisha hafanyi kazi kwa utulivu,
Alikuwa na makali kila alipogusa mpira kuelekea lango letu, ana akili na kasi, kwangu Mimi tulifanya makosa kutomdhibiti.” amesema Paqueta raia wa Brazil.
Mbali na Zouzoua pia Paqueta amemtaja kiungo mshambuliaji wa Young Africans Stephanie Aziz KI alikuwa hatari na mipira yake ya kupenyeza.
“Yule mwenye jezi namba 10 pia (Azizi Ki) alikuwa na mchezo mzuri, alikuwa na pasi za hatari kwenda kwenye eneo letu la ulinzi, tulifanya makosa mengi yaliyotugharimu.”