Lydia Mollel – Morogoro.

Licha ya Mkoa wa Morogoro kuwa na Viwanda vinavyozalisha sukari lakini hali bado sio nzuri kwani wafanyabiashara zaidi ya 100 wamelazimika kupanga foleni ili kununua bidhaa hiyo huku wakilalamika Wakala anayeuza Sukari kuwapendelea baadhi ya watu anaowafahamu.

Wakizungumza na Dar24  Media, Wafanyabiashara hao wamesema wengi wao wamefika majira ya saa 12 asubuhi lakini wanashangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kupita foleni hiyo na kwenda mbele kulipa fedha na kupatiwa Sukari.

Pia Wananchi hao wamelalamikia kitendo cha watu kununua sukari kwa bei ya Shilingi Elfu 72,500  na kuuza kwa zaidi ya laki moja kwani wanawakandamiza wanunuzi wa bidhaa hiyo.

Naye Muuzaji wa sukari hiyo amesema licha ya wafanyabiashara hao kulalamika lakini wao wanawazingatia wafanyabiashara na hakuna upendeleo unaofanyika na kwamba waonalalamika ni wale wanaonunua Sukari wa lengo la kuwauzia watu wengine lakini wao wanawauzia watu wanaotambulika na wale wasiotambulika wanapewa mfuko mmoja au miwili ili kuepusha upandishwaji holela wa Bei.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima aliwataka Wananchi Mkoani humo kuripoti  Bei isiyo halali ya Sukari kwani asilimia 70 ya Sukari inatoka Mkoani Morogoro.

Baada ya miaka 58: Magubike wapata Gari la kubebea Wagonjwa
Paqueta: Pacome, Aziz KI wametuharibia