Bondia Mtanzania, Selemani Kidunda amesema maandalizi kuelekea pambano lake dhidi ya Asemahle Wellem raia wa Afrika Kusini yamekamilika na amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kumpa sapoti.

Pambano hilo la uzito wa Super Walter litakalokuwa la raundi 12, limepangwa kufanyika Machi Mosi katika ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kidunda amesema maandalizi aliyofanya na kujua vizuri mbinu za mpinzani wake vinampa matumaini ya kushinda pambano hilo ambalo anatarajia kuwa na ushindani mkubwa.

“Nataka kuubakiza mkanda wa WBF nchini, hata mashabiki zangu wanapenda kuona hilo na mimi nitahakikisha siwaangushi kwa kushinda kwa pointi za kutosha na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania,” amesema Kidunda.

Bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 10, saba kati ya hayo akishinda kwa KO, amesema ushindi wake katika pambano hilo utakuwa ni salamu tosha kwa mabondia wengine ambao wanatamani kucheza naye.

Ununuzi Meli za Uvuvi, Viwanda uchakataji Samaki mbioni
Uhalifu: Pikipiki zisizo na namba zikamatwe - Madereva Bodaboda