Max Eberl, atakayeanza jukumu kama Mkurugenzi mpya wa Michezo kwenye klabu ya Bayern Munich keshokutwa Ijumaa (Machi Mosi) amesema bado timu hiyo ina matumaini ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Ujerumani pamoja na kuwa nyuma kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Bayer Leverkusen wanaoongoza msimamo wa ligi nchini humo.

Eberl, aliyetumia kipindi cha miaka 15 kama mchezaji kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Bayern na kuwa mchezaji wa kulipwa mpaka mwaka 1994, amewahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa klabu ya Borussia Moenchengladbach kwa miaka 14 kabla ya kujiunga na RB Leipzig mwaka 2022.

Leipzig ilimtimua Eberl mwezi Septemba mwaka jana baada ya kuibuka uvumi unaomhusisha na kujiunga na klabu ya Bayern.

“Ni furaha kurejea hapa baada ya miaka 30, furaha ya kurudi nyumbani,” amesema Eberl.

“Malengo kwenye miezi hii mitatu ni kufanikiwa zaidi kwenye msimu huu. Sio kawaida kuwania ubingwa kuwa nyuma kwa alama nane.”

Tuko nyuma pia kwenye Ligi ya Mabingwa lakini sio kama. haiwezekani kubadili matokeo. Tunaweza penginie hata kuchukua ubingwa. Hauwezi kujua.”

Bayern ambao wiki iliyopita waliamua kuachana na kocha wao Thomas Tuchel ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu, kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo, wako nyuma kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Leverkusen wanaoongoza ligi hiyo.

Ley Matampi afichua siri ya mafanikio
Yusuph Changalawe safarini Italia