Jeshi la Polisi Nchini limetangaza kukemea tabia ya hivi karibuni ambayo imejitokeza kwa baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya vitendo vya kihalifu ambavyo havikubaliki,

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari hii leo Februari 28,2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi, David Misime amesema Februari 21, 2024 huko mkoani Manyara, Wilayani Babati, katika eneo la Magugu, Wananchi wakifanya vurugu na kufunga barabara wakishinikiza Jeshi la Polisi liwakabidhi mtuhumiwa aliyekuwa akituhumiwa kumbaka kisha kumuua mtoto wa miaka saba.

Pia, DCP Misime amesema Febuari 27, 2024, mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe, eneo la Msambiazi, waendesha bodaboda waliteketeza kwa moto basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya safari zake Dar es Salaam Arusha baada ya basi hilo kumgonga dereva wa bodaboda ambaye alifariki dunia.

Amesema, Jeshi la Polisi nchini linatoa onyo kwa baadhi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi kuacha tabia hiyo ambayo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu.

Ameongeza kuwa Kitendo cha kuchoma basi kimedhulumu haki za watu wengine ambao hawakuhusika na tukio hilo la ajali.

Misime amesema, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya waendesha pikipiki za miguu miwili maarufu bodaboda kuacha tabia ya kujichukulia sheria Mkononi

Aidha, meongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka wale wote waliohusika na uhalifu huo wa kuchoma basi Wilayani Korogwe ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 29, 2024
Reliant Lusajo: Nitaibeba Mashujaa FC