Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma imefanikisha upandikizaji wa betri kwenye moyo kwa watu watatu.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa BMH, Daktari Bingwa wa Moyo, Happiness Kusima amesema tayari BMH imefanikisha upandikizaji kwa watu 18 toka kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2021.

Amesema, upandikizaji huu umefanyika kwenye kambi ya Madaktari Bingwa wa Moyo wa BMH kwa kujengewa uwezo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya jijini Dar es Salaam.

Upandikizaji wa betri kwenye moyo ambao kitaalamu unaitwa “pacemakers implantation” unafanyika kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa kwa kawaida ambayo ni 60-100 kwa dakika ambapo wengi wao huwa ni chini ya 40.

Tuzo umahiri wa Uandishi Habari za Wanawake na Uongozi zimewadia
16 wakiwemo waliokatisha masomo kwa ujauzito wabahatika