Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Taifa, Paul Kimiti ameitaka Serikali kutoa ushirikiano kwa Shirika la (TATC) Nyumbu la Kibaha Mkoani Pwani, kwa lengo la kuenzi na kuendeleza malengo ya uundaji wa magari na zana za Kilimo, yaliyoanzishwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julias Kambarage Nyerere ili kujitegemeea kimaendeleo.

Kimiti ameyasema hayo wakati wa Kongamano la Maadili lililoandaliwa na Taasisi hiyo na kufanyika TATC na kuongeza kuwa Baba wa Taifa alitaka kujitegemea kwa kuwa kiwanda Nchini.

Amesema, shirika hilo lilivyo sasa utendaji wake sio kama Baba wa taifa alivyokusudia, kwani kama lingefanya kazi ipasanyo Taifa lingekuwa limepiga hatua kubwa za Maendeleo.

“Sisi Viongozi tukumbushane kwa kuangalia kwamba msingi wa kuanzishwa kwa shirika la nyumbu ni wa kujitegemea unalindwa kwa kuhakikisha tunatimiza ipasavyo malengo yaliyokusudiwa na Hayati Baba wa taifa katika kuliletea taifa Maendeleo yaliyokusudiwa,”  alisema Kimiti.

Aidha, amewataka Watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii kutimiza malengo hayo ya kuanzishwa kwa shirika la nyumbu yanatimia kwa msingi wa ujamaa na kujitegemea.

“Hata vijijini Watu wanaishi kijamaa ingawa wanafikiri ujamaa na kujitegemea ni kuishi masikini lakini sio kweli bali ni wote tuishi kama binadamu katika Umoja kwa kupendana na msikamano wa maendeleo kwa pamoja”

Akifundisha somo la uzalendo katika kongamano hilo, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (NEC-CCM), Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga aliwataka Watumishi wa shirika hilo la Nyumbu kuzingatia itifaki, uadilifu na uzalendo na si kutanguliza maslahi binafsi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Nyumbu na Mkurugenzi wa Nyumbu, Kanali Charles Kalambo amesema Shirika hilo ambalo ni maono ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere limepata mafanikio ikiwa ni pamoja na kubuni gari aina ya Nyumbu ambapo wapo kwenye hatua ya kuanza kuzalisha magari.

Aidha, Kanali Kalambo amesema hivi karibuni wanatarajia kuzindua Mradi mpya na mkubwa wa kuzalisha vipuli vya kuisaidia miradi mikubwa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na vipuli vya Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Julias Nyerere la Rufiji.

Naye Katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani, Abdul Punzi amesema, wataenzi falsafa za Mwalimu Nyerere katika shirika hilo la Nyumbu kwa kufungua Klabu ya Mwalimu Julius Nyerere Nyumbu, ili kwa pamoja waweze kujifunza falsafa na misingi ya Baba wa taifa ya ujamaa na kujitegemea.

Aziz KI: Guede atawashangaza wengi
David de Gea kuibukia FC Barcelona