Nguli wa soka nchini Argentina Sergio Aguero amekanusha ripoti kwamba, atafanya mazezi na klabu ya independiente ya Argentina ili kurudi tena kucheza baada ya kustaafu soka.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Argentina alistaafu soka Desemba 2021 alipokuwa Barcelona akiwa na umri wa miaka 33 kutokana na ugonjwa wa moyo.

“Ni uongo kabisa, sitafanya mazoezi na Independiente,” alisema Aguero.

“Wakati mwingine mambo yanavumishwa tu. Sijui kwa faida ya nani. Narudia tena kuwa daktari wa magonjwa ya moyo alisema niko mzima, nị muhimu kuwa na afya njema. Lakini ili nirudi kwenye mazoezi ya kucheza mpira, nitahitaji kufanyiwa vipimo vingi.”

Mfungaji huyo bora wa muda wote wa Manchester City, Aguero alianza maisha yake ya soka la ujana akiwa na Independiente.

Hivi majuzi Aguero alinukuliwa kwenye Twitch atalazimika kushauriana na daktari wake wa moyo ikiwa kocha wa Independiente, Carlos Tevez atampigia simu.

Tevez alijibu kwamba timu yake ingemkaribisha Aguero kwa mikono miwili.

“Nani hataki kuwa na Kun? Kwanza mimi kama mchezaji mwenzake, na sasa kama kocha,” alisema Tevez kuhusu mchezaji mwenzake wa zamani wa Man City na Argentina.

Lothar Matthaus afuchua ya Xabi Alonso
Joan Laporta ambembeleza Xavi