Kocha, Xabi Alonso atazigomea ofa za Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid zinazomsaka usiku na mchana, kwa mujibu wa gwiji wa Ujerumani, Lothar Matthaus.

Staa wa zamani wa Bayern, Matthaus angependa kuona Alonso anakwenda kuwa kocha mpya wa klabu yake hiyo ya Allianz Arena, lakini anachoamini Mhispaniola huyo atagomea ofa za timu zote zinazomtaka ili abaki Bayer Leverkusen.

Matthaus amesema: “Ndoto zake pengine siku moja kuwa kocha wa Bayern, Liverpool au Real Madrid. Lakini, kwa maoni yangu, bado hajamalizana na Leverkusen.

“Xabi si mtu anayeweza kushawishika na majina makubwa, amefanya hilo kwa kiwango kikubwa sana alipokuwa mchezaji.

“Kitu kingine hatakwenda kushawishika kwa mambo ya kiuchumi. Kitu muhimu kwake ni kitu gani anajenga na anajenga na nani.

“Anafahamu alikotoka na anatambua kuwa ana deni. Na hiyo ndiyo inayonifanya niannini anaweza asiende klabu yoyote msimu ujao.”

Staa huyo wa zamani wa Liverpool, Alonso anaaminika ni miongoni mwa watu wanaostahili kwenda kuchukua mikoba ya Jurgen Klopp wakati Mjerumani huyo atakapoondoka mwishoni mwa msimu huu.

Lakini, klabu yake nyingine va zamani, Bayern, nayo itaingia sokoni kusaka kocha mpya mwisho wa msimu huu kwa sababu kocha Thomas Tuchel ataondoka kwenye kikosi hicho cha Allianz Arena. Na Real Madrid, pia inavutiwa na Alonso.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 2, 2024
Aguero akanusha kurudi uwanjani