Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.
Maambukizi wa Virusi vya Ukimwi – VVU, katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, yamepungua kwa asilimia 0.2 kutoka asilimia 1.6 mpaka asilimia 1.4 katika kwa kipindi cha Oktoba – Desemba, 2023.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Ukimwi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba katika robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2023/2024, kilichofanyika katika Manispaa ya Bukoba, Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Mwajabu Galiatano amesema kwasasa idadi ya maambukizi hayo inaendelea kupungua kutokana na kamati hiyo kuendelea kutoa elimu kwenye jamii, mitaa na kata pamoja na shule.
Amesema, kwa mwaka 2023 katika siku ya ukimwi duniani iliyofanyika Desemba 1 katika uwanja wa uhuru, ilitolewa elimu juu ya maambukizi ya Ukimwi na ukatili wa kijinsia kwenye kata ya Rwamishenye, Kagondo na shule za Omumwani, Hamgembe, Kahororo, Rugambwa, Kashabo, Rwamishenye na Bunena.
“Jumla ya Wanafunzi 3511 walihudhuria na wengine walijitokeza kupima kwa hiyari Virusi vya Ukimwi ambao ni watu 8133 na kati yao wanaume ni 2294 na wanawake ni 5839 huku waliokutwa na maambukizi wakiwa 117 sawa na asilimia 14.