Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuyaenzi maono ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa kusimamia ustawi wa Wananchi, kutenda haki na kuwa mstahamilivu.

Dkt. Samia amesema hayo wakati akihuyuhia Wananchi walioshiriki mazishi ya kitaifa ya Mzee Mwinyi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Amani Abeid Karume.

Amesema kwa ustahamilivu wake wakati wa uongozi, Mzee Mwinyi aliheshimu haki za Binadamu na utawala bora na kuruhusu maoni tofauti ya ukosoaji wa Serikali.

Rais Samia amesema licha ya Hayati Mwinyi kuwa kiongozi katika vipindi vigumu kisiasa na kiuchumi, pia aliweza kuhakikisha utulivu na kufanya mageuzi makubwa katika nyanja za kisiasa na kiuchumi.

Wanawake, Watoto wahanga wakuu ajali za majini
Maambukizi ya Ukimwi yapungua Bukoba