Vifo vya Watu 13 waliofariki Machi 1, 2024 baada ya mtumbwi kuzama Mto Kongo karibu na eneo la mto Lubunga huko Kisangani kwa sehemu kubwa vilioathiriwa ni Wanawake na watoto.
Vifo hivyo, vilitokea baada ya Mtumbwi kupinduka uliokuwa safarini kutoka mji wa Isangi-Makutano, ulioko karibu ya mto Kongo huku ikiarifiwa kuwa idadi ya watu ambayo bado haijajulikana hawajulikani walipo.
Bado haijajulikana sababu za ajali hiyo, lakini Kiongozi wa shirika lisilo la Kiserikali la Sauti ya Lubunga, Crown Isomela alisema mtumbwi huo uligongana na mtumbwi mwingine uliokuwa ukielekea upande wa chini kutoka eneo la Wagenya.
Hata hivyo, mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni mawimbi kutoka maporomoko ya Wagenya, huku Idara ya usalama ya Lubunga ikisema mtumbwi huo pia ulikuwa umebeba zaidi ya watu 30 na mizigo.