Boniface Gideon, Muheza – Tanga.
Shirika la Muheza kwanza limetoa msaada wa vifaa vya kujifungulia kwa akinamama zaidi ya 200 katika vituo vya Afya Mkuzi na Ubwari, vilivyopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Muheza kwanza, Hamis Rajab amesema Shirika hilo linaundwa na Wakazi wa Muheza wanaoishi nje ya Wilaya hiyo na kudai kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango kazi wa Shirika hilo wakuisadia Jamii katika Sekta za Afya,Elimu ,Maji pamoja na uwezeshaji wa kijamii.
Amesema, “sisi ni wazaliwa wa Muheza tunaoishi nje ya Wilaya yetu na wengine wapo nje ya Nchi ,tumejiunda nakuwa Shirika ,lengo letu nikwaajili yakuibadilisha kimaendeleo Wilaya yetu, tumeunda Shirika letu la Muheza kwanza kwaajili yakuisadia Serikali kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wa Muheza.”
Rajabu ameongeza kuwa, vifaa hivyo vya kujifungulia vitawawezesha akinamama zaidi ya mia mbili kupata huduma yakujifungua bila changamoto kubwa na pia wataendelea kusaidia katika kuboresha huduma za Afya, Elimu, Maji pamoja na uwezeshaji wa kijamii.
Akipokea msaada huo, Afisa Utawala Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Nelson Kasiki amesema, “Niwashukuru sana Muheza kwanza ,kwa msaada huu ambao utaenda kuwasaidia akinamama kujifungua Salama,lakini pia niwapongeze kwakujiunda na kutengeneza Shirika ili kuwasaidia wananchi wa Muheza,ni jambo zuri na lakuigwa.
Aidha, amewataka wahudumu wa Afya kufanya kazi kwa weledi kwakufuata miongozo ya Afya na kujiepusha na tabia zinachafua sifa ya huduma za Afya.