Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachoendelea kufanyika jijini Luanda, Angola Machi 4-5, 2024.

Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Kamati ya Fedha Machi 6, 2024 ambapo kwa pamoja vikao hivyo ni maandalizi ya Baraza la Mawaziri litakalofanyika Machi 10 – 11 , 2024 jijini humo.

Aidha, pamoja na masuala mengine vikao hivyo vya awali vitapokea na kujadili taarifa mbalimbali ikiwemo Tathmini ya utekelezaji wa maamuzi ya Mikutano iliyopita.

Hatua iliyofikiwa katika kugharamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC wa 2020–2030, Taarifa ya Kamati ya Fedha, Taarifa ya Kamati ya Rasilimali Watu na Utawala na Hatua iliyofikiwa katika kutafsiri nyaraka muhimu za SADC kwa lugha ya Kiswahili.

Kauli mbiu ya Baraza la Mawaziri la mwaka huu ni ‘’Rasilimali Watu na Fedha: Nyenzo muhimu kwa ukuaji Endelevu wa Viwanda katika Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”.

Muheza Kwanza wawagusa akina mama zaidi ya 200
Vijana wahimizwa kushiriki shughuli za kimaendeleo