Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kamati ya Siasa na Diplomasia (Inter-State Politics and Diplomacy Committee — ISPDC) ya SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao Februari 9, 2024.

Mkutano huo, umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Zambia, Etambuyu Gundersen ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, ulioitishwa, ili kujadili masuala ya kisiasa na Diplomasia katika kanda.

Aidha, Mkutano pia umetoa salamu za pole kwa Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Namibia, kufuatia kifo cha Hayati Dkt. Hage Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichotokea hivi karibuni.

Edward Lowassa afariki Dunia
Kamati ushiriki wa Wazawa Miradi ya Ujenzi yapewa mwezi