Wizara ya Maji imefanya mazungumzo na wadau, taasisi na makampuni mbalimbali ya maji katika eneo la uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha madawa ya kutibu maji nchini lengo likiwa ni kutatua changamoto katika Mamlaka za Maji nchini kutumia fedha nyingi kwa mwaka kwa ajili ya kuagiza dawa za kutibu maji.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameyasema hayo akiwa London,Uingereza kushiriki Mkutano wa 13 wa ubunifu wa teknolojia za maji mwaka 2024(World water Tech innovation summit) iliyoanza tangu juzi Februari 19 hadi 21 Februari 2024.

Amesema, “Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Re Think Events kwa kushirikiana na Idara ya Biashara za Kimataifa ya Serikali ya Uingereza umewaunganisha wadau wa Sekta ya Maji duniani wakiwemo Wafadhili na Makampuni yanayozalisha vifaa vya maji, teknolojia za maji pamoja na madawa ya kutibu maji.”

Mahundi ameongeza kuwa, kupatikana kwa wadau kutoka Taasisi na Makampuni ya kimataifa yatakayowekeza katika viwanda vya kuzalisha madawa ya kutibu maji nchini kutaimarisha huduma za maji nchini kupitia kupunguza gharama za madawa na vitaimarisha uchumi wa Taifa kupitia ajira kwa Watanzania miongoni,” amesema.

Hata hivyo Programu ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Tanzania ni ya miaka nane 2023 – 2030 ambayo itahusisha miradi ya uwekezaji inayohusiana na maji yenye thamani ya takriban Dola za Marekani Bilioni 20.6 na itaongeza wigo wa wadau wa maendeleo na kuongeza bajeti ya ndani kwa ajili ya kuimarisha uwekezaji katika Sekta ya Maji. @wizarayamajitz @maryprisca_mahundi

Madini Tembo kuibua fursa za kiuchumi Nchini
Askari wanne mbaroni kwa kusafirisha Wahamiaji haramu