Mshambuliaji wa AC Milan Rafael Leao, amesisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo siku zijazo, licha ya kudaiwa anawaniwa na klabu za Chelsea na Paris Saint-Germain.

Ripoti ya hivi karibuni ilidokeza kwamba AC Milan inaweza kusikiliza ofa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kuelekeza usajili wa majira ya joto, huku Chelsea ikitajwa kurudisha nia ya kumtaka Leao.

Paris Saint-Germain pia wametajwa kuwa wanajiandaa na maisha bila Kylian Mbappe na hivyo wanamwania Leao.

Hata hivyo, licha ya uvumi huo, Leao ameweka wazi kuhusu mustakabali wake.

“Mustakabali wangu uko Milan. Nipo hapa na bado nina mkataba wa miaka minne” alisema akiiambia Corriere della Sera.

“Milan ilinisaidia nikiwa katika hali ngumu sana, walikaa karibu nami, sisahau, mimi ni mwaminifu, nilifika kama kijana, hapa nilikua kama mtu na mchezaji wa mpira kushinda tena, kichwa changu kiko hapa.”

Ingawa Leao alikiri nia yake ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, alisisitiza kwamba kipaumbele kikubwa ni kuirejesha Milan kileleni cha mafanikio ya Ulaya.

“Ili kukua, lazima nishinde vitu muhimu, kama vile Ligi ya Mabingwa Ulaya au Ligi ya Europa,” alieleza.

“Mambo mazuri husahaulika haraka sana, kwa hiyo lazima ushinde kila mwaka, iwezekanavyo.

Azam wamshika pabaya Prince Dube
PPAA: Malalamiko ya Zabuni kupokelewa kwa mfumo wa NesT