Kocha Xabi Alonso ameripotiwa kuanzisha mazungumzo na Bayern Munich na kuibua hofu huenda akapiga chini mpango wa Liverpool wa kumtaka akarithi mikoba ya Jurgen Klopp.

Mhispaniola huyo yupo kwenye rada za klabu hizo mbili, Bayern Munich na Liverpool wakitaka huduma yake baada ya kufanya kweli akiwa na kikosi cha Bayer Leverkusen huko kwenye Bundesliga.

Kikosi hicho cha Alonso kwa sasa kinaongoza msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Bayern na haijapoteza mechi yoyote msimu huu 2023/24.

Hata hivyo, Bayern wamepanga kuwadhoofisha wapinzani wao hao, Leverkusen kwa kuanzisha mazungumzo ya kumchukua Alonso akawe kocha wao kuanzia msimu ujao.

Bayern imethibitisha itaachana na Thomas Tuchel mwishoni mwa msimu huu. Sasa mjadala ni namna Alonso atakavyokwenda kuwa kocha wao mpya.

Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool alishinda mataji matatu wakati anaichezea Bayer kati ya mwaka 2014 na 2017.

Liverpool nao wanaamini kwa kuwa aliwahi kucheza kwenye timu yao pia, basi wanaweza kumshawishi akatua Anfield kuchukua mikoba ya Klopp, atakayeachana na miamba hiyo mwishoni mwa msimu.

Alonso anafahamnu pengo atakaloacha Klopp kwenye kikosi cha Liverpool ni kubwa sana kuliziba.

Mkataba wa Alonso huko BayArena utafika tamati 2026 na kama kuna timu inamhitaji basi itapaswa kulipa fidia kati ya Pauni 13 milioni na Pauni 21 milioni.

Ally Kamwe: Tunazitaka point zote ligi kuu
Simulizi: Kuwa mtoto wa nje ya ndoa ni zaidi ya mateso