Lydia Mollel – Morogoro.

Katika kuimarisha ulinzi, usalama, kubaini na kutanzua uhalifu, Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata Genge la waalifu zaidi ya 16, ambao wanadaiwa kujihusisha na matukio ya uhalifu wa mtandaoni.

Genge hilo linaongozwa na Elia Charles Sidame (26), ambaye ni mkazi wa Azimio Manispaa ya Morogoro kwa kosa la kufanya biashara hewa mitandaoni na kutoa matangazo ya kutoa ajira na biashara kwa jamii.

 

Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Kamanda wa Polisi Mkoani humo SACP, Alex Mkama amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akikusanya pesa za watu na baada ya hapo hutoweka na kuwaacha pasipo mueleko.

Amesema, watuhumiwa hao wamekuwa wakiwashawishi watu kujiunga na kampuni hewa za Mitandaoni na kuwatoza kuanzia Shilingi Milioni 2 au zaidi, huku wakiwahaidi kupata faida kubwa endapo watawashawishi wengine kujiunga na mtandao huo na badala yake kuishia kutapelewa na kukimbilia kituo cha polisi kuhitaji msaada.

 

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limetoa wito kwa Wananchi kuwa makini na matepeli wa mitandaoni wanaokuja na mbinu mbalimbali na limewaonya vikali wahalifu wote wanaoutumia mbinu mbalimbali kutapeli watu, kwani kila atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mangungu: Msihofu Simba inakwenda Nusu Fainali
Mjadala wa Prince Dube umefungwa rasmi