Scolastica Msewa, Kigamboni.

Waziri wa nchi katika Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jaffo amesema maisha ya mwanadamu yanategemea utunzaji wa mazingira ili kuwa na kizazi endelevu, hivyo ameitaka jamii kupanda miti na kutunza mazingira.

Amesema hayo Kigamboni akiwa amewakilishwa na Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Temeke, Arnold Mapinduzi wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambapo Ofisi ya usimamizi wa utunzaji wa mazingira TEEMO zilizinduliwa.

Amesema, uhai na uendelevu wa binadamu na viumbe wengine hutegemea utunzaji bora wa mazingira tunazungumzia uhai endelevu kati ya binadamu na viumbe hai vingine vinavyoendeleza uhai wa binadamu.

“Binadamu na viumbe vitakosa hewa ya kupumua, vitakosa maji salama ya kunywa na matumizi mengine hata mpaka viwandani ikiwa ni pamoja na kukosa chakula safi na salama na ardhi nzuri na salama ni yule anayeishi kwenye ardhi iliyokosa afya ya udongo,” alisema.

Jafo ameongeza kuwa, “Afya ya udongo ikiathirika hata vyakula hatutapata kwasababu kinachozalisha ni ardhi hii kwani kule kwenye ardhi Kuna viumbe ambavyo havionekani ambao wanakazi ya kurutubisha udongo hapo hata ukidumbukiza kitu kinachooza hakitaoza na mzunguka wa hewa hautafanyika tutakuwa tumeiua ardhi na tutakuwa tumejiua sisi wenyewe.”

Alisema mtu wa mwisho wa kulalamika kuvikosa hivyo vitu ni binadamu kwasababu unapozungumza mazingira bila kutunza mazingira hatuwezi kuona mafanikio yakitimia.

Awali, Mkurugenzi wa Taasisi ya TEEMO na mshauri wa masuala ya mazingira Winfrida Shonde alisema Taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya na kuwezesha jamii katika utunzaji wa mazingira ilikufikisha ajenda ya utunzaji wa mazingira mbele.

Winfrida alisema wanakampeni mbalimbali za utunzaji wa mazingira nchini ikiwemo katika maeneo ya fukwe za bahari ilikuwa na mazingira bora na salama kwa kizazi endelevu.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji avunja ukimya siku ya Wanawake
Ujumbe wa Mhandisi Mahundi kwa Wanawake wote