Lydia Mollel – Morogoro.
Katika kuhakikisha ukatili wa Watoto na Wanawake unatokomezwa, Wanawake Mkoani Morogoro wametakiwa kujitokeza na kuvisemea vitendo ambavyo Watoto wao wanatendewa, bila kujali nani katenda au ukaribu wa mtoto na muhalifu.
Hayo yamesema na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima wakati alipokuwa kwenye madhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kimkoa yaliadhimishwa katika kiwanja cha K-ndege Manispaa ya Morogoro.
Malima, ametoa wito kwa Wazazi kutoona aibu na kusema wazi vitendo wanavyotendewa Watoto kwani wasiposema muhalifu huyo atatenda tena lakini pia amesema wamekubaliana katika kikao na Serikali kuweka mikakati mikali dhiti ya vitendo vya kiukatili hili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa kabisa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebecca Nsemwa amewataka kina Mama kwenda kwenye mikono ya Sheria kupata usaidizi kwani watasaidia kupunguza ukatali wa watoto unaoshamiri mkoani humo.
Mwakilishi wa Wanawake Mkoa wa Morogoro, Sophia kalinga amesema Mkoa Morogoro unashirikiana vyema na Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia katika kuhakikisha kuwa wale wote wanatekeleza vitendo vya ukatili wanachukuliwa hatua, hili kutokomeza vitendo hivyo.
Aidha, katika kuhakikisha huduma kwa waanga wa ukatili inapatika kwa haraka vituo mbalimbali vyakutoa huduma kwa waanga vimeanzishwa (one stop centers) ambapo moja ipo hospital ya sababa na nyingine katika chuo cha Jordan Nanenane.
Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila Mwaka Machi 8 na kauli mbiu ya mwaka huu 2024, ilikuwa ni “WEKEZA KWA WANAWAKE; KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII”.