Wataalam wa Tiba Mbadala, wanaarifu kwamba ukichukua Bamia na ukaziloweka kwenye maji usiku kucha kisha ukayanywa maji yake basi utapata faida zifuatazo kiafya.
1. Bamia imejaa Virutubisho
Virutubisho hivyo ni muhimu kama vile vitamini A, C, na K, pamoja na madini kama Kalsiamu, Magnesiamu na Potasiamu. Kunywa maji ya bamia hukuruhusu kunyonya kwa urahisi virutubisho hivyo, ambavyo ni muhimu kwa afya bora.
2. Bamia ni nzuri kwa viwango vya Sukari kwenye Damu
Bamia ina nyuzinyuzi ambazo zinaweza kusaidia kupunguza kasi ya ufyonzwaji wa sukari kwenye njia ya usagaji chakula, hivyo kuleta utulivu wa viwango vya sukari kwenye damu.
3. Bamia huboresha Afya ya usagaji Chakula
Ute katika bamia na dutu inayonata inayopatikana katika maganda yake hufanya kazi kama ‘laxative’ asilia na inaweza kusaidia kutuliza na kulainisha njia ya usagaji chakula.
4. Bamia inasaidia kupunguza uzito
Ina kalori chache na nyuzinyuzi nyingi, hivyo kuifanya kuwa nyongeza ya mlo kamili na yenye lishe kwa mlo wowote. Kwa kukuza hisia za kushiba na kupunguza matamanio ya njaa, maji ya bamia yanaweza kusaidia kupunguza uzito.
5. Bamia huongeza kinga
Pia ina wingi wa ‘antioxidants’ ikiwa ni pamoja na vitamini C. Kunywa maji ya bamia kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya maambukizi na magonjwa.
Angalizo
Maelezo haya ni taarifa pekee na hayakusudiwi kuchukua nafasi ya ushauri wa kitaalamu wa matibabu, uchunguzi au utabibu.