Young Africans na Simba SC leo Jumanne (Machi 12) zitawafahamu wapizani wao kwenye hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kupitia ‘Droo’ itakayochezeshwa Cairo, Misri.

Timu nyingine ambazo ziko kwenye Droo hiyo ni Al Ahly (Misri), Asec Mimosas (Ivory Coast), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Petro Atletico (Angola), TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Esperance ya Tunisia.

Mechi za awali zinatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 29 na 30 huku marudiano ikipangwa kati ya Aprili 5 na 6.

Kulinganana kanuni za mashindano za Shirikisho la Soka  Barani Afrika ‘CAF’, Simba SC na Young Africans ambazo zilimaliza nafasi ya pili kwenye makundi B na D zitakutana na vinara wa makundi mengine isipokuwa walioongoza makundi yao.

Hivyo Simba SC na Young Africans wanaweza kukutana na timu zote zilizoongoza makundi mengine isipokuwa Asec Mimosas na Al Ahly waliomaliza nafasi ya kwanza kwenye Kundi B na D ambazo wawakilishi hao wa Tanzania walikuwemo.

Simba SC na Young Africans zote zinaweza kupangwa kukutana na mabingwa wa Afrilka wa mwaka 2016 Mamelodi Sundowns.

Kama itatokea Young Africans kukutana na Mamelodi basi hiyo itakuwa awamu ya pili kwa miamba hiyo kuchuana kwani mwaka 2000 mabingwa hao wa soka wa Afrika Kusini waliitoa Young Africans kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuwafunga mabao 3-2 Afrika Kusini kabla ya kutoka sare ya mabao 3-3 CCM Kirumba.

Kama itakutana na Simba SC basi hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Timu nyingine ambayo Simba SC na Young Africans inaweza kukutana nayo kwenye hatua hii ni vinara wa Kundi C, Petro Atletico ya Angola.

Simba SC hawajawahi kukutana na miamba hii ya soka ya Angola lakini Young Africans walikutana nayo kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afika na Young Africans kusonga mbele.

May be an image of 5 people, people playing football, people playing American football and text

Simba SC inaweza kupangwa na Al Ahly ambao kwa miaka ya karibuni wamewahi kukutana mara nne kwenye Ligi ya Mabingwa na mara mbili kwenye Ligi ya Afrika (African Football League).

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Simba SC wameifunga Al Ahly mara mbili zote Uwanja wa Benjamini Mkapa na Al Ahly kupata ushindi mara mbili na kwenye Ligi ya Afrika timu hizo zilitoka sare mara mbili kwenye Ligi ya Soka ya Afrika Oktoba 23, 2023.

Kwenye Droo ya leo, Young Africans na Asec Mimosas wanaweza kukutana ikiwa zimewahi kufanya hivyo mara mbili kwenye hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Young Africans kufungwa mabao 3-0, Dar es Salaam kabla ya kufungwa mabao 2-1 Abidjan mwaka 1998 na mwaka huo, Asec walikuwa mabingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza na ya mwisho kwenye historia yao.

Afya Tip: Faida tano za Bamia kiafya
Simulizi: Nilifukuzwa Chuo kisa kufeli, nimeajiriwa Serikalini