Arsenal wametinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ‘UEFA Champions League’ baada ya kushinda kwa mikwaju ya Penati dhidi ya FC Porto ya Ureno.
Mlinda Lango wa Arsenal David Raya aliibuka shujaa baada ya kuokoa Mikwaju miwili, huku The Gunners wakimaliza ukame wa miaka 14 kufika hatua ya nane bora ya michuano hiyo mikubwa Barani Barani Ulaya.
Gwiji wa Soka wa Klabu ya Arsenal Martin Keown amependekeza kuwa Mlinda Lango huyo kutoka nchini Hispania kuchukuwa mazima nafasi ya Aaron Ramsdale kama kipa chaguo la kwanza.
Keowon amesema baadhi ya Mashabiki walikua hawaamini uwezo wa Mlinda Lango huyo, kutokana na kuwa na mashaka naye hasa alipoanza kuaminiwa na Kocha Mkuu Mikel Arteta.
Amesema Mlinda Lango David Raya amewafanya baadhi ya Mashabiki waliokuwa na mashaka dhidi yake kumuamini baada ya umahiri aliouoinesha kwenye mchezo dhidi ya Fc Porto uliopigwa usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Emirates, jijini London-England.
Raya aliokoa mikwaju miwili ya Penati katika ushindi wa 4-2 dhidi ya FC Porto, baada ya sare ya 1-1 iliyopatikana ndani ya dakika 120.
Raya, ambaye alijiunga na klabu hiyo kutoka Brentford kwa mkopo msimu wa joto, amechukua nafasi ya Aaron Ramsdale kama Mlinda Lango chaguo la kwanza la Mikel Arteta msimu huu 2023/24.
Raya Aliokoa mikwaju iliyopigwa na Wendell na Galeno wa FC Porto, huku Martin Odegaard, Kai Havertz, Bukayo Saka na Declan Rice wakizifumania nyavu za Arsenal.
“Kulikuwa na wasiwasi uwanjani alipoingia kwa mara ya kwanza katika timu ya Arsenal. Unaona sasa, kuna imani kwake na kuna umoja sasa,” Keown aliambia TNT Sports.
“Baadhi ya wafuasi wamemkosoa meneja Arteta kwa kumfanya Raya kuwa nambari moja mbele ya Ramsdale, lakini Keown anafikiri utendaji wake utabadilisha maoni yake.
“Usiku wa leo (jana) unamtia nguvu kwenye timu, ndani ya klabu,” alisema.
Arsenal ilichomoza na ushindi katika mchezo huo wa mkondo wa pili kwa bao 1-0, na kupeleka sare ya dakika za nyongeza, huku Leandro Trossard akifunga bao pekee usiku huo.