Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Imani Kajula amesema mchezo wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Ahly hautakuwa mwepesi, lakini anaamini kikosi chao kina nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kutinga Nusu Fainali kwa mara ya kwanza.

Simba SC imepangwa kukutana na Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Al Ahly ya Misri, baada ya kupangwa kwa Droo ya hatua hiyo jana Jumanne (Machi 12), mjini Cairo-Misri.

Kajula amesema mbali na upinzani mkubwa anaoutarajia, mchezo wao dhidi ya Al Ahly pia utachagizwa na kufahamiana kwa wachezaji wa timu zote mbili, ambazo zilikutana mwaka jana 2023, kwenye Michuano ya African Football League.

Hata hivyo anaamini katika nguvu ya Mashabiki na Wanchama wa Simba SC, ambao siku zote wamekuwa chachu ya mafanikio ya timu yao, hasa inapocheza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

“Itakuwa mechi ngumu kwa sababu tunajuana vizuri na Al Ahly, lakini inatupa ahueni sababu wachezaji wanajuana lakini pia tumecheza Cairo kwenye African Football League”

May be an illustration of American football, football and text that says "#TotalEnergiesCAFCL CAF CHAMPIONS LEAGUE QUARTER FINAL SIMBA SIMBA SC AL AHLY FC IMBA PORTSCLUB"

“Tunajua mechi itakuwa ngumu kwa sababu ya ubora, kimsingi nguvu yetu kubwa itakuwa kwa wachezaji, Benchi la Ufundi lakini zaidi itakuwa nje ya uwanja Kwa sababu ya nguvu ya mashabiki nje ya uwanja na hata kule Cairo”

“Shabiki ni mchezaji wa 12, tunaamini katika nguvu yao na tunakaribisha uwepo wao ili kuufanya mchezo huu kuwa mwepesi” amesema Kajula

Michezo mingine ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu, Young Africans imepangwa kukutana na Mabingwa wa Soka Afrika Kusini Mamelodi Sundown, huku TP Mazembe ya DR Congo ikipewa Petro Atletico ya Angola na baada ya kupangwa kwa Droo ya hatua hiyo jana Espirance ya Tunisia itapapatuana na Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Martin Keown: Raya anastahili heshima Arsenal
Makala: Changamoto za Wanawake zipatiwe ufumbuzi