Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limetoa ufafanuzi wa kuachwa kwa Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta.

Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Hemed Seleman Morocco jana Jumatano (Machi 13) alitangaza kikosi kitakachoshiriki michuano ya FIFA Series 2024, itakayofanyika nchini Azerbaijan.

Kwa mshangao mkubwa jina la Samatta halikutajwa na Kocha Morocco, hali ambayo ilizua maswali na mijadala kwa wadau wa soka la Bongo kupitia mitandao ya kijamii.

Kufuatia mjadala huo ‘TFF’ imetoa ufafanuzi wa kina kuhusu kuachwa kwa Mshambuliaji huyo wa klabu ya PAOK FC, katika kikosi kitakachocheza michezo ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Bulgaria na Mongolia.

Taarifa ya ‘TFF’ imeeleza:  Nahodha wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars”, Mbwana Samatta ameomba kutojumuishwa kwenye kikosi kilichoitwa kwa michezo ya FIFA Series 2024.

Samatta amezungumza na Kocha kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kuomba asijumuishwe katika safari hiyo ya Azerbaijan, ombi ambalo limekubaliwa.

Kikosi hicho kitakachoingia kambini Machi 17, 2024 kitaondoka Machi 18, 2024 na kitacheza michezo miwili na Bulgaria na Mongolia, michezo itakayochezwa Machi 22 na Machi 25, 2024.  Kikosi kinatarajia kurudi Machi 27, 2024.

Kikosi kilichotajwa na Kocha Morocco upande wa Walinda Lango: Aishi Menula, Aboutwaleeb Mshery na Kwesi Kawawa.

Mabeki: Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad, Lusajo Mwaikenda, Haji Mnoga, Mohamed Hussein, Novatus Dismas, Kennedy Juma na Miane Danilo.

Viungo: Feisal Salum, Mudathiri Yahya, Morice Michael, Himid Mao, Yahya Zaydi na Tarryn Allarakhia.

Washambuliaji: Clement Mzize, Saimon Msuva, Kibu Denis Abdul Suleiman, Ben Starkie na Charles M’mombwa.

Diao nje miezi saba hadi tisa
Dkt. Chandika awakumbusha Wananchi kulinda Figo