Shujaa wa kikosi cha Ivory Coast kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ Sebastien Haller atakosa mechi mbili za kirafiki za kimataifa za nchi yake dhidi ya Benin na Uruguay kutokana na majeraha.
Haller, aliyerejea uwanjani baada ya kupambana na saratani, alifunga bao la pili kwenye ushindi wakati Ivory Coast ilipoifunga Nigeria mabao 2-1 kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ mwezi uliopita mjini Abidjan.
Alikosa mechi za awali za Ivory Coast kwenye mashindano hayo kutokana na kuwa majeruhi, lakini alipona na kufunga mabao mawili muhimu ikiwemo lililoipa ubingwa timu hiyo.
Lakini sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 atakuwa nje ya uwanja kwa mara nyingine akiuguza majeraha ya mguu na atakosa mechi mbili za kirafiki za kimataifa tangu kumalizika kwa AFCON 2023.
Machi 23, mwaka huu, Ivory Coast itaikabili Benin na siku tatu baadae watacheza dhidi ya Uruguay katika Uwanja wa Bollaert Delelis, Lens Ufaransa.
Wengine watakaoksa mechi hizo kutoka kikosi kilichoshinda taji la AFCON 2023 kwenye ardhi yao ya nyumbani mwezi uliopita ni nahodha wa timu hiyo, Serge Aurier ambaye Januari alijiunga na Galatasaray akitokea Nottingham Forest na mshambuliaji wa Fiorentina, Christian Kouame anayesumbuliwa na Malaria.
Fae alimjumuisha kwa mara ya kwanza beki wa kulia wa klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa ya Stade Rennais.