Mashirika ya kutoa misaada nchini Haiti, yameripoti Polisi wizi wa vifaa vyao pamoja na misaada vilivyoporwa, wakati huu ambapo nchi hiyo imeingia kwenye wimbi jingine la ghasia za magenge ya Wahalifu.
Hatua hiyo inafuatia magenge hayo ya wahalifu kuvamia Haiti katika wiki za hivi karibuni, kushambulia Taasisi muhimu na kufunga uwanja Mkuu wa Ndege wa Kimataifa.
Machafuko hayo, yamesababisha raia wengi wa Haiti kukumbwa na njaa na kuwaacha wengi katika hali ya kukata tamaa baada ya mamlaka za Serikali kuonesha udhaifu katika kukabiliana na mapigano hayo.
Shirika la kuhudumia Watoto la Kimataifa – UNICEF, lilisema kuwa Kontena lililojaa vifaa muhimu vya msaada pia limeporwa huku Serikali ya Guatemala ikisema kuwa kituo cha ubalozi pia kilivamiwa na vifaa vyake kuibwa.