Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini – TEMESA, kuangalia namna bora ya kuja na ubunifu katika maeneo yao ya kazi, ili kuboresha utendaji kazi.
Naibu Waziri ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Wakala huo ambapo amefanya pia Ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi, uliofanyika Ofisi za TEMESA Makao Makuu jijini Dodoma na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi waliowawakilisha watumishi wenzao kutoka Mikoa na vituo pamoja na Mameneja wa Mikoa.
Amesema wakala unatakiwa kujiendesha kibiashara ili kuongeza pato la Serikali na kuwagiza watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia ushindani wa kibiashara.
”Kuweni wabunifu wa vyanzo vipya vya mapato, wabunifu katika matumizi ya mifumo ya TEHEMA na mbinu mbalimbali za kibiashara, ni vyema tukakumbushana kwamba Serikali,” alisisitiza Kasekenya.
Aidha. amewataka watumishi kuzingatia maadili katika utendeji kazi na kutoa rai kwa watumishi wanaofanya biashara na TEMESA kwa kificho au wazi kwa kupitia kampuni binafsi na kupelekea mgongano wa kimaslahi waache tabia hiyo kwakuwa hawataiwezesha TEMESA kufikia malengo yake waliyojiwekea.