Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa ameielekeza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka – DART, kufikia mwezi Oktoba 2024 iwe imempata mwekezaji binafsi ambaye ni mtoa huduma wa mabasi hayo ili kuleta ufanisi.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Fungu namba 56 na Fungu namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Anne Makinda uliopo bungeni jijini Dodoma.

Amesema, “nilishawambia watu wa ‘DART’ wakati wanakuja kunipitisha kwenye mfumo tunaokwenda nao ikifika mwezi Oktoba wakishindwa kuhakikisha wanampata mwekezaji atayekwenda kuhudumia njia hii wa Private sekta na kushindwa kuhakikisha mabasi yamepatikana waniletee barua za kujiudhuru na tumeshakubaliana na hakuna mjadala watu wanataka huduma.”

Mchengerwa pia amesitiza kuwa kuwepo kwa mwekezaji binafisi katika mradi huo utaendeshwa kwa ufanisi kutokana na kulipa kodi kwa serikali na wakati huohuo atawajibika endapo atatoa huduma isiyostahili.

Hata hivyo, Mchengerwa amesema Septemba hadi Oktoba, Serikali itakuwa imepata mabasi ya kutosha ya kuendesha njia zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi ili watanzania wa Dar es Salaam waweze kuhudumiwa vizuri kabla ya kuanza kupeleka huduma ya mwendokasi katika majiji mengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Denis Londo amepongeza uamuzi huo na kusema kuwa maamuzi hayo yaacha alama nzuri wa Waziri aliyepo kutokana na ubunifu huo.

TEMESA yatakiwa kuboresha utendaji kazi
Mwaseba jela miaka 25 kwa kukutwa na Dawa za kulevya