Anaitwa Elisabeth Demidoff, Mwanamke kutoka uzao wa familia ya Wanaviwanda wa Urusi ambao walipata pesa zao kwa kuuza Chumvi na manyoya.
Aliolewa na Mrusi Nikolai Nikitich Demidoff, ambaye pia alikuwa mrithi wa utajiri wa viwanda kutoka kwa familia yake, lakini jkwa bahati mbaya, ndoa yao ilivunjika, na wenzi hao walitengana.
Baada ya hapo, Elisabeth alienda kuishi Paris lakini ilipofika mwaka 1818 akiwa na umri wa miaka 40 aliaga Dunia. Ingawa maisha yake hayakuwa ya kukumbukwa, lakini ombi lake la mwisho lilikuwa ni la kushangaza. upande.
Inasemekana kwamba baada ya kifo chake, jamaa zake walishtuka kugundua kwamba aliacha wosia akiarifu kwamba urithi wake wa mamilioni ya pesa apatiwe mtu ambaye angeweza kukaa mwaka na siku moja katika kaburi lake.
Mtu huyo alitakiwa kuketi kando ya jeneza lake kwenye makaburi ya Père Lachaise huko Paris na Watu wengi walijaribu bila mafanikio kukaa katika kaburi hili ili kupata utajiri wa haraka, lakini hakuna aliyewahi kufanikisha kutokana na mauzauza.
Hata hivyo inaarifiwa kwamba maombi yaliendelea kutumwa kwa wale waliotaka kujaribu Bahati ya kupata mamilioni hadi miaka ya 1900, ingawaje haakuna taarifa rasmi iwapo mshindi alipatikana.