Anaitwa Sarah Rector, Binti mdogo zaidi na Mmarekani mwenye asili ya Afrika kuwahi kuwa tajiri mkubwa akiwa na umri wa miaka 18 pekee mwaka 1920. Alizaliwa mwaka 1902 katika mji ambao waliishi watu weusi katika eneo la Taft lililopo Kansas City, mashariki mwa jiji wa Oklahoma.
Lakini mkasa wake ni moja ya visa ambayo vinadhihirisha chuki ya watu wa weupe dhidi ya watu weusi. Inarifiwa kuwa Binti huyu aliwahi kupewa ardhi ekari 159.14, isiyo na rutuba, tofauti na Wazungu ambao wao walipatiwa ardhi nzuri kwa ajili ya Kilimo.
Umiliki wa ardhi hiyo, ulimlazimu Sarah kulipa kiasi cha dola 30 kama kodi ya ardhi kwa kila mwaka, jambo ambalo lilikuwa ni gumu sana kwake, hivyo akatangaza kuuza ardhi yake. lakini alifanyiwa figisu hadi akashindwa kuuza ardhi hiyo, hivyo akalazimika kuendela kuilipia kodi.
Katika uhangaikiaji wa namna ya kuweza kumudu ulipaji wa kodi ya ardhi, Februari 1911, Baba yake Sarah akaitoa ardhi hiyo kwa makubaliano ya muda mrefu kwa Kampuni ya uchimbaji Mafuta ya Standard Oil, ambapo baadaye mwaka 1913 kampuni hiyo ikaanza kuchimba mafuta, na ghafla ardhi hiyo ambayo haikutakiwa ikaanza kupanda thamani.
Hapo familia ya Sarah ikaanza kupata fedha nyingi kila mwaka, huku Sarah akipata fedha nyingi zaidi. Utajiri ukawa mkubwa na akawa maarufu sana, lakini kwa hila za Wazungu wakaona mtoto kwa rangi nyeusi hawezi kuwa tajiri kiasi kile. Wakachapisha makala kwenye gazeti kueleza kisa cha utajiri wake, ila wakimuelezea kama mzungu, na sio mtu mweusi.
Utajiri wake ulimpa ofa kubwa za mikopo, mialiko mikubwa ya kidunia, zawadi mbalimbali na alikuwa akimiliki hisa na bondi, nyumba ya kulala wageni, duka la mikate na Mkahawa huko Muskogee, Oklahoma, ekari 2,000 za ardhi na ofa nyingi za posa zilimfikia Wanaume wakitaka kumuoa.
Hata hivyo, aliolewa na Mfanyabiashara wa magari Homer Roberts na kuhamia Chicago, huko wakafungua kampuni ya Roberts-Campbell Motors, kampuni ya pili ya uuzaji magari inayomilikiwa na Mwafrika, ambapo hata hivyo uzaji wa magari mapya ulidorora na kuanza kwa unyogovu na ubia ukafungwa na walitalikiana, baadaye aliolewa tena na William Crawford.
Lakini kwa kipindi hicho, watu weusi walinyimwa huduma muhimu kama za kupanda Treni, hadhi ya kusafiri na Ndege daraja la kwanza nk. Lakini kwa sbabu za kipesa waliona Sarah anaweza kupata huduma zote hizo, hivyo Bunge la Oklahoma likapitisha sheria kumtambua Sarah kama mzungu, ili aweze kunufaika na huduma hizo.
Julai 22, 1967 Sarah aliaga Dunia akiwa na umri wa miaka 65. Mabaki yake yalizikwa katika makaburi ya jiji la Taft, sehemu ambayo alizaliwa.