Mastaa sita wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Young Africans wanatarajia kujiunga na wenzao kesho Alhamis (Machi 28), kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi (Machi 30).

Wachezaji hao waliokuwa kwenye majukumu na timu za taifa ni Mlinda Lango Djigui Diarra (Mali), Viungo Stephan Aziz Ki (Burkina Faso), Pacome Zuozoua (Ivory Coast) na Mshambuliaji Kennedy Musonda (Zambia).

Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ally Kamwe amesema walishafanya utaratibu wa kuhakikisha wachezaji hao wanawahi kurudi na kupata siku mbili za kufanya mazoezi na wenzao.

Tumefanya mawasiliano na viongozi wa mashirikisho na wametuhakikishia hadi kufikia Alhamisi (Machi 28) tayari watakuwa wamerejea na hizo ni habari njema kwetu sababu tunahitaji kuwa na kikosi kamili kuelekea mechi yetu dhidi ya Mamelodi,” amesema Kamwe.

Mbali na nyota hao, wachezaji wengine wawili waliokuwa na timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Azerbaijan, ni Beki na Nahodha Bakari Mwamnyeto na Mlinda Lango Abutwalibu Mshery pia watajiunga na wenzao.

Akizungumzia umuhimu wa mchezo huo, Kamwe amesema mbali na kusaka historia mpya ya klabu hiyo kwenye michuano hiyo lakini pia wanaweza kuvuna kiasi kikubwa cha fedha kama wataingia hatua ya Nusu Fainali.

Rushwa yamponza Chen Xuyuan
MAKALA: Asiye bahati alivyobahatika