Boniface Gideon, Tanga.
Kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga chini ya mwenyeki Rajab Abdurrahman, kimebaini madudu kwa baadhi ya miradi ya kimkakati Wilaya ya Pangani,
Miradi iliyobainika kuwa na dosari ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani ambapo mkandarasi anayetekereza Mradi huo amepaua Bati mpya kwenye paa yenye mbao chakavu,ucheleweshwaji wa makusudi Ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Mwembeni pamoja na Ujenzi wa chini ya kiwango Barabara ya lami yenye urefu wa km 3.
Aidha Mwenyekiti Rajab pamoja na mfanyabiashara maafu Nchini Azim Dewj kila mmoja amechangia sh.Mil.10 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mwembeni pamoja na Sh.mil.2 na ununuzi wa tofali 3000 ili kuwezesha ujenzi wa Zahanati ya Kata Mikinguni.
Akizungumza na Wakazi wa Vijiji vya Mkwaja,Mikinguni,Madanga (Mwembeni),na Stahabu, Mwenyekiti WA CCM mkoa Tanga,amesema Kuna baadhi ya watumishi wilayani humo wamekuwa ni wazembe kwenye utendaji wao wa majukumu ya kazi hali inayosababisha baadhi ya miradi kudorola kwenye ujenzi na mingine imekuwa chini ya kiwango.
“Hapa kuna uzembe kwa baadhi ya watumishi,na hawa ndio wanasababisha chuki za Wananchi dhidi ya Serikali na chama, Wilaya hii imechezewa sana na kuanzia sasa hatutaki kuchezewa tena , tunataka Pangani mpya, tunataka miradi ya maendeleo itekerezwe kwa wakati,” alisisitiza Rajab.
Awali akikagua miradi hiyo, Rajab aliwataka Wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha inamalizika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu,
“Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga kinaelekeza kuwa kuanzia sasa, miradi yote inayosuasua na ile inayoendelea tunataka ikamilike kwa wakati ili Wananchi wapate huduma kwa urahisi, kwenye hili ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani,tumepokea mil.900 lakini naona Kuna mchezo unataka ufanyike ,haiwezekani milango na paa ikawa na mbao chakavu,lakini pia Barabara ya ndani ya Jiji haijamaliza hata mwaka tayari imeshaanza kuharibika,hii haikubaliki kabisa” Alisema Rajab.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mussa Kilakala, Alisema ameyapokea maagizo yote ya chama nakuahidi kuyafanyia kazin mapungufu yaliyopo kwenye miradi yote,
“Nimepokea maelekezo yote ya chama, kwaniaba ya Watendaji wa Serikali Wilaya ya Pangani tunaahidi kuwa tunaenda kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye miradi ya maendeleo inayoendelea, niwaahidi tu kuwa miradi hii itakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi” Alisema Kilakala.