Serikali Nchini, imesema itaifanyia kazi Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikati – CAG, pamoja na taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU.
Kupitia taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pia ameahidi kuiwasirisha Bungeni ndani ya muda mfupi kwa mujibu wa Katiba kwa kuwa ripoti hizo zinasaidia kuimarisha utendaji kazi wa Serikati na Mashirika ya Umma pamoja na kujirekebisha.
Licha ya kwamba ni takwa la kikatiba, Rais Samia amesema uwasilishaji wa Ripoti hiyo ni kuimarisha uwazi na uwajibikaji ambayo ni hatua ya awali kabla ya kusikia majibu ya Serikali, kuhusu dosari zote zilizoainishwa.
Rais Samia ameagiza marekebisho yaliyofanyika kutokana na ripoti zilizopita kwani yamesaidia kupatikana kwa asilimia 99 ya hati safi na asilimia moja pekee ya hati chafu kwa kuwa ripoti hizo zinachagiza kuongezeka mapato na kwamba dosari zilizotolewa zitafanyiwa kazi na Serikati na ni matumaini yake kuwa hazitajirudia katika ripoti zijazo.