Wizara ya afya ya Kenya, imewatahadharisha Wananchi wake kuhusu uwepo wa homa kali ya mafua, ambayo inaendelea kusambaa kote nchini humo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya afya Dkt. Patrick Amoth amesema homa hiyo kali kwa kawaida husambaa msimu wa Februari na Machi, huku akiwataka walio na dalili za homa hiyo kujitenga ili wasiambukize wengine.
Homa ya mafua ni ugonjwa wa kuambukiza unaojulikana pia kwa jina lenye asili ya Kiitalia influenza na kwa kifupi chakeni ni flu, ingawa kwaKiswahiliunaitwa pia kaputula au Homa ya kaptura kwani ugonjwa huo uliingia Afrika Mashariki pamoja na kaptura.
Dalili za homa ya mafua ni pamoja na kikohozi, maumivu shingoni, maumivu ya misuli, maumivu ya kichwa na homa na wakati mwingine lakini si kwa kawaida, kunatokea pia kutapika na kuhara.
WAKATI HUOHUO.
Idara ya afya katika Kaunti ya Mombasa, imeripoti kuzuka kwa maradhi ya Pneumonia au homa ya mapafu kwa watoto wachanga, huku visa zaidi ya 10 vikiwa vimeripotiwa kwa mji wa Mombasa.
Afisa wa afya ya umma wa Serikali ya Kaunti Dkt. Abdallah Deleno amesema visa hivyo vimethibitishwa katika eneo bunge la Likoni na Nyali.