Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amezielekeza Halmashauri zote Tanzania Bara
kupanda miti pembezoni mwa barabara, ili kuipendezesha miji na kuhifadhi mazingira.

Dkt. Jafo ametoa maelekezo hayo wakati akizindua ‘Mradi wa Twiga wa Kijani’ unaohusisha zoezi la upandaji wa miti katika shule za 60 za mikoa sita ya Tanzania, leo Machi 28, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Jeshini, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Amesema, Tanzania imekuwa ikitembelewa na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani hususan baada ya kuzalishwa kwa filamu ya ‘Royal Tour‘ na Serikali kununua ndege nyingi zaidi hivyo ni muhimu tukatengeneza madhari ya kuvutia pembezoni mwa barabara kwa kupanda miti.

Waziri Dkt. Jafo ameyataka majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Mbeya, Arusha na Dodoma kuwa ya mfano wa kuigwa katika kutekeleza maelekezo ya kupandwa miti pembezoni mwa barabara na kuwaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa
kusimamia zoezi la usafi katika maeneo yao kwa kuwa na wakandarasi wa usafi wenye vifaa bora.

Uchaguzi Mei 29: Tume yamkalia kooni Zuma
Wananchi watahadharishwa uwepo homa kali ya Mafua