Tume ya uchaguzi ya nchini Afrika Kusini, imemzuia rais wa zamani wa Taifa hilo Jacob Zuma kuwania kiti chochote kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Mei 29, 2024.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mosotho Moepya amesema hatua hiyo imetokana na pingamizi kutoka kwa baadhi ya raia kutaka Zuma kuzuiwa kuwania wakidai hafai baada ya kuhukumiwa kifungo jela kwa zaidi ya miezi sita mwaka 2021.

Zuma amekuwa akijihusisha na chama cha uMkhonto we Sizwe, ambacho wengi wanadai huenda kitatoa ushindani mkali kwa chama tawala cha ANC kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo, sheeria inamruhusu Zuma kukata rufaa na anao muda wa kufanya hivyo kwa kuainisha sababu ambazo anadhani zitansaidia kutengua katazo hilo la Tume ya uchaguzi.

Amnesty yalia na ukiukwaji haki za Binadamu
Dkt. Jafo: Halmashauri zipande Miti pembezoni mwa Barabara