Chama cha Umkhonto we Sizwe (MK) cha Afrika Kusini, kimekishutumu Chama tawala cha ANC kwa kuhusika katika tukio la ajali iliyompata Kiongozi wao Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliyenusurika katika ajali ya gari usiku wa kuamkia Ijumaa Machi 29, 2024.

Ajali hiyo, ilitokea ikiwa ni muda mchache baada ya Maafisa wa Uchaguzi kumzuia Zuma kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Mei 29 na hivyo kuzua hali ya mvutano.

Polisi wa Afrika Kusini walisema gari la Zuma liligongwa na mtu mmoja mwenye umri wa miaka 51 ambaye alikamatwa katika Jimbo la KwaZulu Natal kwa kosa kuendesha gari akiwa amelewa na uzembe barabarani.

Msemaji wa chama cha MK, Nhlamulo Ndhlela amesema katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, Zuma amenusurika katika ajali mbili zinazowahusisha madereva wanaodaiwa kuwa walevi.

Amesema wamekuwa kikifuatilia kwa karibu mlolongo wa matukio ya kufanana yanayomtokea Zuma chini ya utawala wa Cyril Ramaphosa, mara baada ya Zuma kutangaza atafanya kampeni kwa tiketi ya chama cha MK ili kugombea urais.

 

Makazi ya Waziri Mkuu yashambuliwa kwa bomu
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 1, 2024