Watu ambao bado hawajafahamika, wanadaiwa kushambulia kwa mabomu makazi ya Waziri Mkuu wa Libya, Abdulhamid al-Dbeibah Machi 31, 2024 tukio ambalo halikusababisha maadhara.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa, Waziri mmoja wa Serikali ya Libya alithibitisha kwamba shambulizi hilo lilisababisha uharibifu mdogo bila ya kutoa maelezo zaidi.

Libya imezongwa na machafuko tangu mwaka wa 2011 baada ya kuzuka kwa uasi ulioungwa mkono na jumuiya ya kujihami ya NATO pamoja na kugawanyika kwa taifa hilo mwaka 2014.

Baadhi ya Wananchi wakisimulia tukio hilo, wamesema walisikia milipuko mikubwa karibu na bahari ya eneo la kifahari la Hay Andalus mjini humo, ambalo ni makazi ya Kiongozi huyo Dbeibah ambapo baadaye vikosi vya usalama viliwasili.

Hitilafu Gridi ya Taifa chanzo kukosekana kwa Umeme
Ajali ya Zuma: Rais Ramaphosa Atajwa