Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniface Butondo hii leo April 2, 2024 Bungeni jijini Dodoma, ameibana Serikali ieleze ni lini Mahakama ya Wilaya ya Kishapu itajengwa, huku akisema mpango huo ulikuwa kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024.

Katika swali lake, Mbunge Butondo aliuliza kuwa, “katika mwaka wa fedha 2023/2024 ilionesha kwamba Wilaya ya Kishapu itajengewa Mahama ya Wilaya, ni lini ujenzi huo utaanza kufanyika?.”

Akijibu swali hilo, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana amesema, “Mheshimiwa Spika kimsingi Mahakama ya Wilaya ya Kishapu ni miongoni mwa zile Mahakama ambazo zipo katika mpango mkakati wa kujengwa mwaka 2024/2025.”

Amesema tayari Kamati ya Sheria na Katiba imepitisha pesa na Mahakama hiyo ipo katika maandalizi ya mchoro na mzabuni amekwisha kutangazwa ili kumpata mkandarasi wa ujenzi.

CRDB mdhamini mpya Kombe la Shirikisho
Babati mwenyeji fainali Kombe la Shirikisho